Mtandao wa Twitter unafanyia marekebisho sheria zake ili kuwarahasishia kazi watumiaji wake na kuufanya uwe wa kuvutia kwa wale wanaojiunga nao kwa mara ya kwanza.
Wanachama wa mtandao hao sasa wataweza kuongeza kile wanachochapisha kwenye mtandao huo, zikiwemo picha na video bila ya kuathiri kiwango cha sasa cha maneno 140 ambayo mtu anastahili kuandika.
Twitter pia itafanya marekebisho kuhusu jinsi watu wanaweza kuwasiliana katika mtandao.
Mdadisi mmoja anasema kuwa hatua hizo zinaashiria mwelekeo mwema, lakini akaongeza kuwa wameangazia suala moja tu ambalo ni kuongeza watumiaji wake.
Licha ya mtandao huo kutumiwa sana katika masuala yanayohusu habari mwaka uliopita, umekuwa na wakati mgumu kuwavutia watumiaji wapya suala ambalo linatajwa kuchangiwa na ugumu ulio katika kuutumia.
Anasema kuwa tatizo kuu ni kuwavutia watumiaji wapya na kuwafanya wawe wazalendo kwa mtandao. Anaendelea kusema kuwa bado Twitter haijalishughulikia hilo.
Source: BBC
0 comments:
Post a Comment