Thursday, May 26, 2016

Ndege inayotumia nguvu za jua yafanya safari ya mwisho

Solar Impulse Two inatumia nguvu za jua
Ndege inayotumia nguvu za jua imeondoka kutoka magharibi mwa Marekani inapoanza awamu yake ya mwisho ya safari katika jaribio la kuizunguka dunia.

Safari hiyo ya 12 inayofanywa na ndege hiyo inayojulikana kama Solar Impulse Two, ni kutoka jimbo la Oklahoma kwenda mji wa Dayton jimbo la Ohio.

Safari hiyo inatarajiwa kuchukua muda wa saa 17.

Source: BBC

Twitter kufanyiwa mabadiliko ili kuwavutia watumiaji


Mtandao wa Twitter unafanyia marekebisho sheria zake ili kuwarahasishia kazi watumiaji wake na kuufanya uwe wa kuvutia kwa wale wanaojiunga nao kwa mara ya kwanza.

Wanachama wa mtandao hao sasa wataweza kuongeza kile wanachochapisha kwenye mtandao huo, zikiwemo picha na video bila ya kuathiri kiwango cha sasa cha maneno 140 ambayo mtu anastahili kuandika.

Twitter pia itafanya marekebisho kuhusu jinsi watu wanaweza kuwasiliana katika mtandao.

Twitter imekuwa na wakati mgumu kuwavutia watumiaji wapya suala ambalo linatajwa kuchangiwa na ugumu ulio katika kuutumia.
 Mwanzilishi mwenza wa Twitter na mkurugenzi mkuu Jack Dorsey, aliiambia BBC kuwa lengo lao ni kuhakikisha kuwa wakati watu wanapoutumia unaonekana kuwa ulio na maana.

Mdadisi mmoja anasema kuwa hatua hizo zinaashiria mwelekeo mwema, lakini akaongeza kuwa wameangazia suala moja tu ambalo ni kuongeza watumiaji wake.

Licha ya mtandao huo kutumiwa sana katika masuala yanayohusu habari mwaka uliopita, umekuwa na wakati mgumu kuwavutia watumiaji wapya suala ambalo linatajwa kuchangiwa na ugumu ulio katika kuutumia.

Twitter pia itafanya marekebisho kuhusu jinsi watu wanaweza kuwasiliana katika mtandao.
 Brian Blau, ambaye ni mchambuzi kutoka shirika la Gartner, anasema matatizo yanaoikumba Twitter kuwapata watumiaji wapya hayawezi kutatuliwa na mabadiliko hayo.

Anasema kuwa tatizo kuu ni kuwavutia watumiaji wapya na kuwafanya wawe wazalendo kwa mtandao. Anaendelea kusema kuwa bado Twitter haijalishughulikia hilo.

Source: BBC

Vita kati ya Huawei na Samsung mahakamani

Huawei
Kampuni ya teknolojia ya Huawei inaishtaki Samsung kuhusu madai kwamba haki zake zimekiukwa.

Kampuni hiyo ya China imesema kuwa inaishtaki Samsung kupitia mahakama mbili moja ikiwa California na nyengine ikiwa Shenzhen.

Kulingana na Huawei,simu zake kadhaa pamoja na programu zake ilizobuni zimetumiwa katika simu za Samsung bila ruhusa yake.

Samsung

Samsung imeambia BBC itatetea maslahi ya bishara zake.
Hatahivyo programu zinazodaiwa kuibwa na Samsung hazijatangazwa.

Source: BBC